New Amaan Complex
Simba SC

Simba, Yanga na Azam Kuhamia New Amaan Complex Msimu wa 2026/27

Vardo November 5, 2026 9:03 am

Klabu za Simba SC, Yanga SC, na Azam FC zimeungana na kuwasilisha maombi rasmi ya kutumia Uwanja wa New Amaan Complex uliopo Zanzibar kama uwanja wao wa nyumbani kwa ajili ya mechi za hatua ya makundi ya mashindano ya klabu Afrika msimu wa 2026/27.

Hatua hii imefikiwa kufuatia changamoto ya upatikanaji wa viwanja vinavyokidhi vigezo vya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF). Kwa sasa, Uwanja wa Benjamin Mkapa upo kwenye matengenezo makubwa, huku Uwanja wa Uhuru ukihitaji maboresho zaidi ili kukidhi viwango vya kimataifa vinavyotakiwa na CAF.

New Amaan Complex Tayari Kupokea Mechi za CAF

Uongozi wa New Amaan Complex umethibitisha kupokea maombi ya klabu hizo na kueleza kuwa uwanja huo tayari umefanyiwa maboresho makubwa pamoja na tathmini ya CAF, hatua inayouweka katika nafasi nzuri ya kuandaa mechi hizo za kimataifa.

Kwa mujibu wa kanuni za CAF za mwaka 2022, mechi za hatua ya makundi zinapaswa kuchezwa katika viwanja vya Daraja la Tatu (Category 3), vinavyokidhi vigezo vya:

  • Usalama wa mashabiki na wachezaji.

  • Miundombinu ya kisasa ya uwanja.

  • Vifaa na mazingira bora ya matangazo ya televisheni.

Uwakilishi wa Tanzania Kimataifa Msimu wa 2026/27

Maombi haya yatakapokubaliwa, mashabiki wa soka Zanzibar watapata fursa ya kushuhudia mechi kabambe za klabu za Tanzania katika anga la kimataifa:

  • Simba SC: Inatarajia kushiriki hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya saba.

  • Yanga SC: Inatinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya tano.

  • Azam FC na Singida Black Stars: Zitaiwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho Afrika, zikicheza hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo.

Wydad Yatajwa Kumfuatilia Libasse Gueye wa Simba Simba SC Yaweka Mikakati Mizito Mapumziko ya FIFA: Kambi Na Mechi za Kirafiki Kupikwa