Libasse Gueye Aongoza Assists Ligi Kuu 2026/27 | Simba SC
Winga wa kimataifa wa Simba SC, Libasse Gueye, ameendelea kuonyesha kiwango bora na cha kuvutia katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27, baada ya kukamata namba moja kwenye orodha ya wachezaji wenye pasi nyingi za mabao (assists).
Nyota huyo raia wa Senegal amefikisha jumla ya assists saba (7), hatua inayothibitisha mchango wake mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya Simba SC na kumfanya kuwa mmoja wa wachezaji hatari zaidi ligi kuu kwa sasa.
Takwimu za Assists Ligi Kuu ya NBC:
Kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizotolewa na bodi ya Ligi Kuu Tanzania, orodha ya wachezaji wanaeongoza kwa pasi za mabao ni kama ifuatavyo:
-
Libasse Gueye (Simba SC) – Assists 7
-
Hussein Zakouani (Singida Black Stars) – Assists 4
-
Maxi Nzengeli (Yanga SC) – Assists 3
-
Khalid Aucho (Yanga SC) – Assists 3
-
Haruna Chanongo – Assists 3
-
Ani Elijah – Assists 3
-
Rashid Chambo – Assists 3
-
Jeancy Mboma – Assists 3
Silaha Muhimu kwa Simba SC
Uwezo wa Libasse Gueye wa kutengeneza nafasi za mabao na kuwapa wenzake mipira ya mwisho umekuwa chachu kubwa kwa Wekundu wa Msimbazi katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu na mashindano mengine msimu huu.
Gueye ameonyesha kuwa si mfungaji pekee bali ni injini ya kutengeneza mashambulizi ya timu hiyo. Kadiri ligi inavyoendelea, winga huyo ana nafasi kubwa ya kuendeleza rekodi yake na kuiongezea Simba SC makali zaidi katika mechi zijazo.