Uchaguzi Simba SC 2027: Tarehe Rasmi na Mkutano Mkuu Kutangazwa
Klabu ya Simba SC imetangaza rasmi tarehe ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kawaida wa wanachama wake, ambao miongoni mwa ajenda zake kuu zitakazojadiliwa ni pamoja na uchaguzi wa viongozi wapya watakaoongoza klabu hiyo kwa kipindi kijacho.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu, mkutano huo unatarajiwa kufanyika Jumamosi, Januari 30, 2027, kuanzia saa 3:00 asubuhi. Eneo rasmi litakolofanyika mkutano huo litatangazwa baadaye.
Batua na Katiba ya Simba SC
Mkutano huu umeidhinishwa kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 21(1) ya Katiba ya Simba Sports Club ya mwaka 2018 (iliyofanyiwa marekebisho Novemba 2025), pamoja na Ibara ya 20(5) ya tarehe 18 Februari, 2026.
Uongozi wa klabu hiyo umeeleza kuwa ajenda mahsusi pamoja na eneo la mkutano zitatangazwa rasmi kulingana na matakwa ya Ibara ya 21(2) ya katiba ya klabu.
Mchakato wa Uchaguzi na Usimamizi wa TFF
Ajenda inayovuta hisia na kusubiriwa kwa hamu kubwa na wanachama ni uchaguzi wa viongozi, utakaofanyika chini ya Ibara ya 20(6) na 22(i) ya Katiba ya Simba.
Mchakato mzima wa uchaguzi utasimamiwa kikamilifu na Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Taratibu, kanuni, na maelekezo mengine yanayohusu jinsi ya kushiriki au kugombea yatatolewa kwa wanachama kadiri mchakato unavyoendelea.
Mkutano huu unatajwa kuwa wa mabadiliko makubwa ndani ya Msimbazi, ukitoa fursa pana kwa wanachama kujadili mwelekeo, maendeleo, na uendeshaji wa timu kuelekea msimu ujao.