Uncategorized

KKUNGO HATARI MPYA YANGA AAHIDI KUMALIZA KAZI NA TSHISHIMBI

admin June 2, 2019 7:49 am


BAADA ya juzi kusaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Yanga, kiungo mshambuliaji mpya Mnyarwanda, Issa Bigirimana ‘Walcott’ amemuulizia Ibrahim Ajibu akitaka kujua anabaki au anaondoka Jangwani.

Bigirimana alisaini mkataba huo juzi baada ya kufi kia makubaliano mazuri na viongozi wa Yanga kabla ya kumpa mkataba huo akitokea APR ya Rwanda aliyokuwa anaichezea.

Bigirimana alisema kuwa, anavutiwa na wachezaji wengi Yanga, lakini zaidi ni Ajibu ambaye alimmwagia sifa nyingi kuwa ni mchezaji anayemkubali kutokana na kiwango kikubwa alichokuwa nacho.

“Wapo wachezaji wengi ninaowakubali Yanga lakini huyu jamaa anayevalia jezi namba 10 (Ajibu) anajua sana na ningefurahi kuona ninacheza naye timu moja kwenye msimu ujao.

“Mwingine ni Tshishimbi yule kiungo mwenye rasta, ninampenda sana anacheza kwa kutumia akili nyingi na ufundi mwingi, ninaamini nikicheza naye pamoja tutatengeneza kitu kizuri ndani ya Yanga,” alisema Bigirimana.

SIMBA MSIMU UJAO NI ZAIDI YA SIFA, ASILIMIA 99 KAHATA KUMWAGA WINO – VIDEO NIYONZIMA AVUNJA UKIMYA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply