Home Uncategorized ALIYETAJWA KUTUA YANGA MAMBO YAGEUKA, WASHINDWANA ‘ PESA NDOGO’

ALIYETAJWA KUTUA YANGA MAMBO YAGEUKA, WASHINDWANA ‘ PESA NDOGO’


Imeelezwa kuwa beki aliyemaliza mkataba na klabu ya KMC, Ally Ally amesema kuwa maslahi ndiyo kikwazo kilichomfanya asisaini mkataba na klabu ya Yanga.

Taarifa imeeleza kuwa Ally amedai Yanga walimpa dau dogo lililopelekea mpango huo kushindikana na sasa Beki huyo anaangalia uwezekano wa kusaini timu nyingine au kusalia KMC

“Yanga walikuja na tulikaa nao mezani shida ni dau.

“Mimi mpira ndiyo maisha yangu, siwezi kucheza kwa maslahi madogo nina ndugu wananiangalia mimi.

“Sina mkataba na timu nyingine yeyote, naendelea na mazungumzo na kuna baadhi ya timu zimenifuata.”

Imeandaliwa na Yossima Sitta Jr

SOMA NA HII  NDANDA YATOSHANA NGUVU NA SIMBA NANGWANDA