Uncategorized

POLOKWANE FC WAIKOMALIA SIMBA ISHU YA BOCCO

admin June 15, 2019 5:03 am


KAMA mipango ikienda sawa huenda nyota wa Simba, Adam Salamba akatua Afrika Kusini kukipiga klabu ya Polokwane FC.

Dili hilo limekuja baada ya dili la mshambuliaji John Bocco kuingia doa kwa kile kilichoelezwa kwamba Polokwane FC walimsainisha mchezaji kimakosa hivyo wameamua waikomalie Simba iwape mchezaji mmoja kwa mkopo.

Uongozi wa Simba kupitia Mtendaji Mkuu, Cresesteus  Magori umesema kuwa kumtoa Bocco ni ngumu hasa kutokana na malengo ya klabu ya Simba kwa sasa kuwa ya kimataifa.

“Kumtoa mchezaji kama Bocco kwa sasa ni ngumu hasa ukizingatia Simba ni timu kubwa hivyo kumpeleka Afrika Kusini bado sio sahihi, hilo limeisha na viongozi wa Polokwane wameelewa na kwa sasa wanahitaji mchezaji wetu mmoja kwa mkopo,” amesema.

Mchezaji huyo ambaye Polokwane wamemuomba imeelezwa kwamba ni Adam Salamba. 

AJIBU KUTANGAZWA SIMBA LEO LEO NDIO LEO, KUBWA KULIKO KUFANA, MOJA KWA MOJA AZAM TV

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply