Uncategorized

ZAHERA ABADILI UPEPO YANGA

admin June 20, 2019 9:01 pm


BOSI wa benchi la ufundi la Yanga, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo amewasisitiza viongozi wa timu hiyo kuwapa mikataba mipya kwa haraka wachezaji waliomo kikosini humo ambao wamemaliza na wapo kwenye malengo yake.

Yanga hadi sasa tayari wameshawasajili wachezaji wa timu za nje ambao ni Sadney Urithob, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana, Maybin Kalengo, Juma Balinya, Lamine Moro, Selemani Mustapha na Abdulaziz Makame.

Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla amesema; “Kocha Zahera ameagiza kwamba kwa sasa ni kuwabana wachezaji waliopo kwenye timu kwa kuwapa mikataba mipya kwa wale ambao anawahitaji kwa msimu ujao.”

“Tayari ameshatoa orodha yake ambapo nalo tutalifanya kama ilivyokuwa kwa wachezaji waliokuwa nje ya timu. Tutamalizana nao na muda siyo mrefu tutaanza kuwatangaza kama ilivyokuwa kwa hawa,” alisema Msolla.

STARS YAPEWA RAI YA KUCHUKUA KIKOMBE MISRI, LAZIMA IFUATWE WACHEZAJI SIMBA WAGOMA KISA MPUNGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply