Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali ‘Mzee Akilimali’ ambaye ni Katibu ameunga mkono hoja ya Rostam na kusema Yanga haiwezi kumilikiwa na mtu mmoja.
“Kwa kweli mimi nimefurahishwa na kauli ya Rostam na ninamkubali sana kwani klabu kubwa kama Yanga ambayo ina wanachama wengi huwezi kuimilikisha na mtu mmoja kwani kufanya hivyo ina maana kila kitu atakuwa nacho yeye.
“Mimi jana nilimsikiliza mwenyewe na timu kama Yanga inatakiwa iongozwe na wanachama sasa kama mwanachama umeenda pale na kudhani kuwa kuna mdhamini uache kuchangia basi wewe hufahi kuwa mwanachama, mwanachama unatakiwa uchangie.”
Kauli ya Akilimali imekuja mara baada ya Rostam kuibuka na kusema anataka kuifadhili Yanga kupitia makampuni yake na si kuimiliki.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.