Mchezaji mwingine kutoka Brazil mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya beki wa kati na kiungo mkabaji, Gerson Fraga Vieira (26) amesaini mkataba wa miaka miwili na Simba SC.
Vieira ambaye amewahi kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 17 ya Brazil iliyokuwa na wachezaji maarufu kama Neymar, Philippe Coutinho, Casemiro na golikipa Alisson.
Feaga pia alicheza timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 20 na alicheza klabu kadhaa za Brazil ikiwepo GrĂªmio amejiunga na klabu yetu akitokea ATK FC ya India.
Usajili umefanyika mara baada ya jana wekundu hao wa Msimbazi kumuongezea mkataba mwingine wa miaka miwili beki wake Mohammed Hussein “Tshabalala”.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.