Home Uncategorized Juuko siyo aina ya mchezaji wa Simba!

Juuko siyo aina ya mchezaji wa Simba!

Kuna mengi yanazungumziwa sana kwa sasa baada ya michuano ya Afcon kuanza. Tanzania tunalalamika, Kenya walalamika lakini Uganda wanafurahia.

Wako katika mazingira mazuri kwenye michuano hii ndiyo maana wanafurahia. Wameanza vizuri michuano hii, wamempiga Congo magoli 2-0.

Katika ushindi huo kuna wachezaji wawili wa Simba ambao walionesha kiwango kikubwa. Emmanuel Okwi ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo na Juuko Mursheed.

Baada ya mechi hiyo mijadala ilikuwa kwanini Juuko Murshid kutokupewa nafasi kubwa kwenye kikosi cha Simba wakati ni beki mzuri.

Ni ukweli Juuko ni mchezaji bora lakini siyo aina ya mabeki ambao wanatakiwa kucheza katika timu ya Simba chini ya Patrick Aussems.

Mwalimu Patrick Aussems amekuwa akiwatumia mabeki wa kati ambao wanauwezo wa kuanzisha mashambulizi kwa kupiga pasi kwa kuanzia nyuma.

Hiki kitu hakipo kwa Juuko Murshid. Ndiyo maana anaonekana kutopata nafasi katika kikosi cha Simba kwa sababu ya kutoendana na aina ya uchezaji wa timu ya Simba.

The post Juuko siyo aina ya mchezaji wa Simba! appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AWAPA NENO HILI MASTAA SIMBA