UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa kwa sasa hauna mpango wa kusajili wachezaji kutoka nje ya nchi kutokana na kuamini uwezo wa wachezaji wa ndani.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa klabu haina hesabu za kusajili nyota wa kigeni.
“Kwenye klabu yetu haitatokea tukasajili wachezaji wa kigeni, sura zao itakuwa ni ngumu kuonekana kwetu kwa kuwa tuna imani na wachezaji wa ndani.
“Kwa sasa tumeanza majaribio ya wachezaji wa ndani tukiwa na lengo la kusuka kikosi kipya hivyo tutawasili kwa kadri watakavyoonyesha uwezo wao,” amesema.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.