Home Uncategorized MAALIM BUSUNGU: LIKIJA DILI KUBWA NASAINI

MAALIM BUSUNGU: LIKIJA DILI KUBWA NASAINI


MAALIM Busungu mshambuliaji wa zamani wa timu ya Lipuli amesema kuwa kwa sasa yupo tayari kurejea kucheza mpira iwapo timu itatokea timu itakayompa dau la maana.

Busungu amesema kuwa kwa sasa yupo Dodoma akiendelea na shughuli za kilimo na hajaacha mpira kwa kuwa ndio kazi yake.

“Siwezi kuacha kucheza mpira kwa kuwa ni kazi yangu, kwa sasa nimepumzika huku Dodoma naendelea na shughuli zangu za kilimo, ikitokea timu yenye dau zuri nasaini,” amesema.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA