Uncategorized

CAF YAIRUHUSU SIMBA KUTINGA JEZI YA KIJIVU

admin July 16, 2019 11:32 am


UONGOZI wa Simba umesema kuwa msimu ujao Simba watatumia jezi ya rangi nyekundu nyumbani na rangi nyeupe ugenini huku wakitumia rangi ya kijivu pale timu zinapogongana rangi.

Mtendaji mkuu wa timu ya Simba, Crecentius Magori amesema kuwa mpango huo ni kutokana na utaratibu wa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) 

“Timu imeweka kambi nchini Afrika Kusini ikiwa ni maalumu kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao kwenye ligi pamoja na michuano ya kimataifa.

“Kuhusu jezi simba itatumia jezi nyekundu nyumbani, jezi Nyeupe ugenini na jezi za kijivu ambayo ni natural (halisi) kwa mazingira yeyote endapo timu zitakuwa zimevaa jezi zinazofanana,” amesema.

DIDA; NINA OFA TANO MKONONI KWA SASA HILO DAU LA LEROY SANE WA MANCHESTER CITY LAZIMA UKAE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply