Uncategorized

SIMBA YAKIRI KUTOMLIPA MCHEZAJI MURSHID MSHAHARA WA MIEZI MIWILI, YATAJA SABABU

admin July 16, 2019 6:35 am

UONGOZI wa Simba umesema kuwa ni kweli unadaiwa na mchezaji wao Juuko Murshid anayecheza timu ya Taifa ya Uganda ila haina mpango wa kuachana naye kizembe.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori amesema kuwa, Murshid ni mtoro wa timu anapaswa arejee haraka kabla ya kuchukuliwa hatua.

“Tunadaiwa na Murshid mshahara wa miezi miwili, haina maana tunashindwa kumlipa hapana, yeye ametoroka kambini hivyo hauwezi kumlipa mshahara mfanyakazi mtoro.

“Kwa sasa popote alipo anatakiwa arejee kazini akishindwa tutamchukulia hatua mpaka Fifa kwa kuwa tumemuandikia barua hajatujibu, hivyo tunalishughulikia suala hilo kwa ukaribu,” amesema.

NGASSA: TUTAPAMBANA KIUKWELI MSIMU UJAO HUYU NDIYE PILATO WA FAINALI YA AFCON KATI YA SENEGAL NA ALGERIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply