Uncategorized

KIONGOZI YANGA AACHANA NA SOKA, AKIMBILIA KWENYE MUZIKI, ADAI SOKA HALILIPI

admin July 17, 2019 9:01 pm

Ikiwa ni takribani siku kadhaa sasa zimepita tangu kuachia ngazi kwa aliyekuwa Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali ‘Mensa’, mchezaji huyo wa zamani wa Yanga amesema ameamua kuingia kwenye muziki.


Mensa ambaye amekuwa akijulikana kwa mbwembwe nyingi katika wadhifa wake, ameamua kuingia kwa muziki akisema kuwa unalipa kuliko soka.

“Nataka niwambie kuwa muziki una hela, nimeamua kuingia huko.

“Muziki ni kazi yangu namba mbili ukiachana na mpira, naamini nitafanya vizuri tu.”

Pondamali amesema licha ya kuachana na masuala ya soka, atazidi kuipenda Yanga kwa kuendelea kuwa mwanachama kama kawaida na si kuwa amejitoa kabisa ndani ya klabu hiyo.

MZEE KILOMONI WALA HAJAPOA, AJA NA TAMKO LINGINE ZITO JUU YA HATI SIMBA, MAGORI ATAJWA SONSO AVUNJA UKIMYA, AAMUA KUFUNGUKA BAADA YA KUTEMWA STARS NA NDAYIRAGIJE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply