Uncategorized

MZEE KILOMONI WALA HAJAPOA, AJA NA TAMKO LINGINE ZITO JUU YA HATI SIMBA, MAGORI ATAJWA

admin July 17, 2019 9:01 pm


Mzee Hamis Kilomoni ambaye mpaka sasa amekuwa akisisitiza kuwa hajaondolewa kwenye Baraza la Wazee wa Simba, amefunguka na kusema hatishwi na kauli za viongozi wa klabu hiyo.

Kilomoni ameamua kufunguka kuwa anatarajia kutoa kauli yake ya mwisho wiki hii atakapoitisha kikao na waandishi wa habari.

Maamuzi ya kuitisha kikao hicho yametokana na tamko la Ofisa Mtendaji wa Simba, Crescentius Magori ambaye juzi alisema kuwa Kilomoni wala hana hati ya Simba hivi sasa.

Magori aliamua kuweka wazi kuwa Kilomoni amekuwa akiwadanganya watu kuwa hati ya klabu hiyo anaishikilia lakini si kweli kwa kuwa tayari mahakama imeshatoa tamko huko hatambuliki.

Kufuatia tamko la Magori, Kilomoni ameeleza kuwa atazungumza na wanahabari na akieleza Magori kuwa ni mtu wa kawaida ndani ya Simba wala hajatishika naye.

MASHABIKI WANAAMINI DEMBELE ATAPELEKWA NA GRIEZMANN LIVERPOOL KIONGOZI YANGA AACHANA NA SOKA, AKIMBILIA KWENYE MUZIKI, ADAI SOKA HALILIPI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply