Uncategorized

HUYU NDIYE ALIYE NYUMA YA USAJILI WA NYOTA WA SIMBA FRANCIS KAHATA

admin July 18, 2019 3:06 am


FRANCIS Kahata kiungo mpya wa Simba amesema kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wamechangia kumshawishi ajiunge ndani ya kikosi hicho ni mshambuliaji Meddie Kagere.

Kahata amejifunga kwa kandarasi ya miaka miwili ndani ya Simba akitokea timu ya Gor Mahia ambayo Kagere naye aliwahi kuitumikia.

“Nilikuwa nina ofa nyingi mbali na Simba kutokana na ukubwa wa klabu na ukaribu wangu na Kagere sikuona haja ya kwenda mbali nikakubali kujiunga na Simba.

“Kwa sasa ninafuraha kwa kuwa nimeona timu ipo vizuri na ina mipango mingi mizuri hivyo kwa kushirikiana nao nina amini tutafanya vema,” amesema Kahata.

REAL MADRID KUUZA NYOTA WATANO KUMPATA NYOTA WA MANCHESTER UNITED MANCHESTER UNITED: HAKUNA OFA YA PAUL POGBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply