Uncategorized

MANCHESTER UNITED: HAKUNA OFA YA PAUL POGBA

admin July 18, 2019 7:01 am
OLE Gunnar Solskjaer, meneja wa Manchester United amesema kuwa bado atabaki na nyota wa kikosi hicho Paul Pogba na anaweza kumfanya akawa bora zaidi kwa kuwa hakuna ofa inayomtaka.
United wana kazi ya kumzuia Pogba ambaye anawindwa na Juventus pamoja na Real Madrid huku wakiwa wametaja dau kubwa la kumuza mchezaji huyo la pauni milioni 170.
Pogba na wakala wake Mino Raiola hawajaweka siri mpango wa Pogba kutaka kusepa United msimu ujao.
“Nitampa changamoto mpya na ninaweza, Paul ni mchezaji mzuri na bora hana tatizo lolote na kama atacheza kwa mtindo ule kama wakati ninakuja ndani ya kikosi hiki atakuwa bora zaidi.
“Siwezi kusema chochote kuhusu hatma yake kwa kuwa kumekuwa na mazungumzo mengi juu yake na ninajua kwa dhati kipi ambacho Paul anafikiria na mpaka sasa hatuna ofa yoyote juu yake,” amesema.
HUYU NDIYE ALIYE NYUMA YA USAJILI WA NYOTA WA SIMBA FRANCIS KAHATA LIGT AUNGANA NA CR7 JUVENTUS, ASAINI MIAKA MITANO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply