Uncategorized

KUMEKUCHA SIMBA, MO AMALIZA UTATA MAZIMA

admin July 27, 2019 8:40 pm

KAULI ya Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji leo imetoa ile hofu ya mashabiki kuhusu hatma yake ndani ya Simba.

Baada ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr.Harrison Mwakyembe kuzungumza juu ya umiliki wa timu kuhusisha wawekezaji zaidi ya watatu lilizua maswali mengi huku mashabiki wakihoji hatma ya Mo bila kupata majibu.

Hivyo leo Mo kupitia ukurasa wake wa Instagram maneno yake yamevunja ule utata na kuondoa hofu kwa mashabiki.

Ujumbe wake ulikuwa unasomeka namna hii: “Nimesikitishwa na mijadala mitandaoni ya kumshutumu Waziri Mwakyembe kwamba ameanzisha utaratibu mpya wa mwekezaji kuwa na 49% na wanachama 51% ya hisa. Ndugu zangu, si kweli. Utaratibu huu upo tangu 2017 kisheria na sisi Simba tulikubali.

“Waziri Mwakyembe alituruhusu Simba tuendelee na mwekezaji mmoja. Ndugu WanaSimba Mimi nipo na niko na nyinyi, siendi popote. Na sasa tumeishazungumza na Serekali na mazungumzo ni mazuri. Nawasihi WanaSimba wote twendeni tukaishangilie Timu ya Taifa na tukutane Simba Day tarehe 6. Tulianza vizuri na Serikali na tutamaliza vizuri na Serikali,”.

SIBOMANA WA YANGA APANIA MAKUBWA STAA MPYA YANGA YAMKUTA MAKUBWA, ISHU YA SAUZI IPO LAIVU NI KESHO NDANI YA SPOTI XTRA JUMAPILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply