Uncategorized

VITA YA SIMBA KWENYE ENEO LA ULINZI YAACHWA KWA MBELGIJI

admin July 27, 2019 10:35 am
PASCAL Wawa,beki wa Simba amesema hana hofu na nafasi yake ndani ya kikosi hicho, kazi ni kwake kupambana kisha kocha Aussems ndiyo ataamua ampange nani.
Wawa ndani ya Simba atapambania namba na Gerson Fraga, Kennedy Juma, Erasto Nyoni na Yusuph Mlipili.

 Simba kwa sasa imepiga kambi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.
“Kikosi chetu kina mabadiliko kwenye safu ya ulinzi, lakini hilo haliwezi kunipa hofu mimi kwamba siwezi kupata nafasi, sababu najua mwalimu ataamua nani acheze kutokana na kuangalia kiwango bora kati yetu, ndiyo maana sina hofu.
“Kama sasa maandalizi yanakwenda safi kabisa, hali ya hewa nzuri, hivyo kila kitu kipo sawa na kocha amekuwa akifanyia kazi sana eneo la ulinzi kwa bidii kuweka mambo sawa, ili kuwa na safu bora ya ulinzi,” amesema.
SIMBA YALAZIMISHA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA HAWA NDIO WAPINZANI WA SIMBA KIMATAIFA HATUA YA AWALI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply