Uncategorized

SIMBA WABEBA IMANI KUBWA KWA MASHABIKI

admin July 29, 2019 9:38 pm

OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa hawana hofu na mchezo wao watakaocheza jumanne siku ya Simba day mashabiki wa Simba wanajua wanachokitaka.

Agosti sita Simba itacheza uwanja wa Taifa na timu ya Power Dynamo mchezo wa kirafiki wenye lengo la kuwatambulisha wachezaji wake wapya na wale wa muda mrefu.

“Haijalishi itakuwa ni jumanne watu wanasema hawatakuja watu sisi tunajua kwamba wana Simba wanapenda kuiona timu yao hivyo nawaomba wanasimba wanunue tiketi mapema ili kupunguza ule msongamano wa kujazana siku ya mwisho.

“Tumejipanga tunajua kwamba watu wanataka kumuona Kahata, wale Wabrazili pia wote watakuwwepo bila kumsahau Meddie Kagere, na wachezaji wengine wote, ni wakati wetu wa kutamba sasa,” amesema.

CAF YATEUA WAAMUZI SITA WA ONGO KUCHEZESHA MECHI ZA LIGI YA MABINGWA NA SHIRIKISHO HIVI NDIVYO CAF WALIVYOTIBUA MIPANGO YA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply