Uncategorized
SIMBA YAMALIZANA NA KIFAA KUTOKA TP MAZEMBE, KILIWAHI KUCHEZA KOMBE LA DUNIA
Kazi ya kusajili wakali watakaohakikisha kikosi cha Mabingwa kinazidi kuwa tishio kwa wapinzani inaendelea.
Mshambuliaji raia wa Congo DR, Deo Kanda (29) amejiunga na Mabingwa wa nchi Simba SC.
Kanda amesaini mkataba wa mwaka mmoja kukipiga Msimbazi akitokea TP Mazembe ambapo alikuwa mmoja wa wachezaji ambao waliiwezesha kushinda Ubingwa wa Afrika mwaka 2009, 2010 (aliifungia goli kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Esperance) na 2013.
Kanda pia akiwa ameshiriki Kombe la Dunia la Vilabu mwaka 2009, 2010, 2013.

Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.