Home Uncategorized AMUNIKE AENDELEZA DHARAU, ASISITIZA HANA CHA KULAUMIWA

AMUNIKE AENDELEZA DHARAU, ASISITIZA HANA CHA KULAUMIWA



Na Saleh Ally, Cairo
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike ameendelea kusisitiza kwamba yeye hana cha kulaumiwa.

Amunike amesema mara baada ya Stars kupoteza mchezo wake wa mwisho katika michuano Afcon.

Taifa Stars ilifungwa mechi zote tatu za michuano hiyo kwa kukubali mabao nane katika mechi tatu huku ikifunga mawili.

Baada ya mechi ya mwisho baada ya Stars kulala kwa mabao 3-0 kutoka kwa Algeria, Amunike amuse a hana cha kulaumiwa.

“Nilaumiwe kwa lipi? Mimi ni kocha na timu uliiona. Hapo ndipo tulipofikia na nilichofanya sikuwa na zaidi ya kuongeza,” alisema.

Hata alipoulizwa kwamba ana maanisha hakuwa na uwezo wa kuongeza chochote cha kuiokoa au ana maanisha hakuwa na uwezo zaidi ya hapo, akajibu.

“Mimi nimemaliza, indigo tulipofikia, ahsante.”

MECHI ILIZOPOTEZA TAIFA STARS:
Vs Senegal 2-0
Vs Kenya 3-2
Vs Algeria 3-0

SOMA NA HII  SABABU YA YANGA KUWEKA KAMBI MAPEMA MORO YATAJWA