Uncategorized

YANGA: TUPO KAMILI GADO KUTOA BURUDANI KWA MASHABIKI SIKU YA MWANANCHI

admin August 2, 2019 1:37 am

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa unatambua ushindani utakavyokuwa Agosti 4, mbele ya kikosi cha Kariobangi Sharks ila wamejipanga kutoa burudani,

Dismas Ten, Kaimu Katibu wa Yanga amesema kwa sasa kila kitu kinakwenda sawa namaandalizi kwa wachezaji yapo sawa.

“Siku ya kilele cha siku Mwanachi itakuwa ni siku ya burudani ya kipekee na timu yetu inaendelea kufanya mazoezi chini ya Kocha Mkuu, mwinyi Zahera.

“Wapinzani wetu si watu wa mchezemchezo tunatambua ubora wao kwani Everton walinyoosha mikono kwao hivyo nasi tuna kazi kubwa ya kufanya, pia walifanya vizuri kwenye michuano ya SportPesa.

“Wito wangu kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi kuona namna tutavyotoa burudani kwani kuhusu vifaa na jezi zote halisi zitakuwepo pamoja na mpango mzima wa kuwatambulisha wachezaji wetu,” amesema.

Everton  na Kariobangi zilicheza mchezo wa kirafiki dakika 90 zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na kupelekea kupigwa penalti ambapo Kariobangi ilishinda penalti 4-3

HIKI NDICHO KIPO NYUMA YA MTIBWA SUGAR KUSHUSHA VICHAPO MECHI ZA KIRAFI DUH!KUMBE KIPIGO CHA POLISI TANZANIA NI SALAMU KWA WAETHIPOA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply