Uncategorized

RC: PAUL MAKONDA AWAPA TANO YANGA, ATAJA KITAKACHOUKUZA MPIRA WA BONGO

admin August 5, 2019 8:11 am


PAUL Makonda, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, amesema kuwa yeye ni kwa haua ambayo Yanga wameanza kwa sasa ni hatua kubwa na inahitaji pongezi.

Yanga jana walihitimisha siku ya Mwananchi kwa kucheza mchezo wa kirafiki na Kariobangi Sharki uwanja wa Taifa na walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Makonda amesema”Naona Yanga wameanza vizuri na wamerejea kwenye ubora wao nimeongea na viongozi na nimewapongeza kwa jambo ambalo wamelifanya.

“Mimi ni mpenzi wa Yanga, shabiki wa Azam, mkereketwa wa KMC lakini mwanachama wa Simba.

“Tunaamini wameanza vizuri lakini timu hizi kubwa ambazo ni Yanga, Simba, Azam na KMC zikifanya vizuri imani yetu mpira wetu utakwenda mbali sana,” amesema.

PSG YAMKOA NEYMAR JR, YAGOMA KUTOA KWENDA BARCELONA BUNJU KUMENOGA, DR.MWAKYEMBE, MO WAFANYA UKAGUZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply