Uncategorized

YANGA: KIKOSI CHA KAZI HIKI LAZIMA TUTUSUE MWANZO MWISHO

admin August 6, 2019 11:31 am


MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kikosi chake kwa sasa kimetengamaa hivyo hana mashaka na ushindani wa msimu ujao pamoja na mechi za kimataifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Zahera amesema kuwa kikubwa ambacho kinampa jeuri ya kupata matokeo chanya ni upana wa kikosi chake kwa sasa.

“Kikosi changu kwa sasa kina wachezaji makini ambao wanajuhudi wakiwa uwanjani, nina imani msimu ujao tutakimbizana sana na wapinzani wetu bila kuchoka.

“Kila mmoja anapenda kuona kikosi kikifanya vizuri ila haina matatizo ndivyo itakavyokuwa kwani wote wana morali ya kufanya kazi,” amesema. 

Nyota wapya ambao wamesajiliwa na Yanga kwa ajili ya msimu ujao ni pamoja na Patrick Sibomana, Juma Balinya, Mapinduzi Balama, Ally Ally na Maybin Kalengo.

JUVENTUS, REAL MADRID WAPIGANA VIKUMBO KUINASA SAINI YA POGBA NYOMI KAMA LOTE TAIFA SIMBA DAY, TIMU ZAWASILI, WALE WA BUKU TANO TIKETI ZIMEKATA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply