Uncategorized

MK 14 APIGA PICHA NA MCHEZAJI MPYA KIRAKA WA SIMBA KIPENZI CHA MASHABIKI

admin August 7, 2019 2:36 pm


MOHAMMED Dewji, ‘Mo’, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugezi ndani ya Simba leo ameweka picha yake kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na mshambuliaji wa kimataifa, Meddie Kagere ‘MK 14’.

Jana kwenye utambulisho wa wachezaji wapya wa Simba, Mo alitambulishwa kama mchezaji mpya ambaye anacheza namba zote uwanjani kuanzia golikipa, beki, mshambuliaji na kiungo.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema: “Sasa namleta kwenu mchezaji mpya wa Simba ambaye anacheza nafasi zote, kuanzia ushambuliaji huko anafunga, golikipa, beki yeye namba zote anacheza naye ni tajiri wetu Mo,”.

Baada ya kusema hivyo mashabiki wote wa Simba walishangilia kwa furaha mwanzo mwisho.

MSHAMBULIAJI WA YANGA AWAPANIA TOWNSHIP ROLLERS NYOTA MPYA WA YANGA, RAIA WA RWANDA ATUMIKA KWENYE UTAPELI, AFUNGULIWA AKAUNTI NNE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply