Uncategorized

NYOTA MPYA WA YANGA, RAIA WA RWANDA ATUMIKA KWENYE UTAPELI, AFUNGULIWA AKAUNTI NNE

admin August 7, 2019 3:07 pm

KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga, Mnyarwanda, Issa Bigirimana ‘Walcott’ amekiona cha moto baada ya ‘wahuni’ kufanya utapeli kwa kutumia akaunti yake.
Mnyarwanda huyo ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao, wengine baadhi ni Patrick Sibomana, Maybin Kalengo, Farouk Shikalo na Sadney Urikhob.
Sibomana amesema kuwa watu wasiojulikana wametengeneza akaunti ‘fake’ ya Instagram wanaoitumia vibaya kuwatapeli baadhi ya mashabiki wa Yanga baada ya kusajiliwa na kutangazwa mchezaji wa Yanga  amewatahadharisha mashabiki wa Yanga kuwa makini na matapeli hao wanaotaka kujipatia fedha kwa kutumia jina lake.
  
“Labda niwatajie akaunti yangu ninayoitumia kwenye akaunti zangu za Instagram na Facebook kuwa natumia Issa Walcott na siyo Issa Bigirimana, ni vema wakalifahamu hilo katika kuepuka kutapeliwa na vibaka.
“Zipo akaunti nne ‘fake’ zilizotengenezwa na wezi hao ambazo siyo zangu, wanazitengeneza kwa nia mbaya ya kutaka kuwaibia mashabiki wa Yanga kwa kuwaomba fedha.
“Niwaombe hao wezi kuachana na hizo akaunti, sitaki kuona hili likiendelea la wizi wa fedha na mashabiki wa Yanga hiyo nyingine ndiyo akaunti yangu,” amesema
MK 14 APIGA PICHA NA MCHEZAJI MPYA KIRAKA WA SIMBA KIPENZI CHA MASHABIKI WANNE KMC WA KIMATAIFA KUIKOSA AS KIGALI, KISA CAF

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply