Uncategorized

ISHU YA MGOMO WA BEKI KISIKI WA YANGA, KELVIN YONDANI IPO NAMNA HII

admin August 8, 2019 3:34 pm


MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hakuna tatizo kati ya Yanga na beki kisiki Kelvin Yondani kwani ameomba ruhusa kutokana na matatizo ya kifamilia aliyonayo.

Yondani mpaka sasa hajajiunga na wachezaji wenzake kambini, visiwani Zanzibar licha ya kukamilisha majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ huku taarifa zikidai kwamba ana mgomo wa wazi.

Zahera amesema kuwa:”Yondani najua kwamba ni mchezaji muhimu ila kwa sasa yeye yupo likizo kwani aliniomba ruhusa kuna masuala yake anashughulikia hivyo akimaliza atajiunga na timu itakaporejea.

“Nimekubaliana naye hasa ukizingatia kwamba ana mambo ya muhimu ambayo anapaswa kuyafanya akikamilisha kazi tukirudi Dar ataungana na timu hivyo kwa sasa sisi tunajiaanda naye anaendelea kumalizia matatizo yake hakuna mgomo,” amesema.

TANZANITE YATINGA JUMLA FAINALI COSAFA, YAWAPIGA MABAO 2-0 AFRIKA KUSINI YANGA KUMENOGA, SIMBA NAKO KAMA KAWA, KESHO NDANI YA CHAMPIONI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply