Uncategorized

SIMBA IPO BIZE NA MCHAKATO WA KUIREJESHA MIKONONI MWA WATU, KILA MMOJA KUWA SEHEMU YA MAFANIKIO

admin August 8, 2019 1:34 am


MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba, Mohammed Dewj ‘Mo’ amesema kuwa anapenda kuona timu ya Simba inafikia hatua kubwa ya mafanikio kitaifa na kimataifa.

Mo amesema kuwa mpango ambao upo kwa sasa kati ya uongozi ni kuirejesha timu mikononi mwa watu ili nao wawe sehemu ya historia ya mafaniko ya kikosi hicho.

“Naipenda timu ya Simba na ninawapenda mashabiki pia wa Simba, kwa sasa tunafanya mchakato kuwafanya wananchi wawe sehemu ya mafanikio ya Simba kwa kuwaruhusu nao wachangie fedha kwa ajili ya kkamilisha shughuli za maendeleo ya Simba ikiwa ni pamoja na ujezi wa uwanja wa Bunju pamoja na mambo mengine.

“Maono yetu kwa pamoja ni kuona Simba inafikia hatua kubwa ya uwekezaji kama ambavyo wenzetu wanafanya nje kwani nimejifunza mambo mengi nilipokuwa huko na ni wakati wa kuona kwamba kila mmoja anakuwa sehemu  ya mafanikio,” amesema Mo.

POLISI TANZANIA: MSIMU UJAO MAMBO YATAKUWA MOTO, MDHAMINI MKUU PASUA KICHWA NYOTA HUYU AANDALIWA KUWA MRITHI WA DAVID SILVA NDANI YA MANCHESTER CITY

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply