Uncategorized

YANGA: HAKUNA TIMU YENYE REKODI YA KUJAZA UWANJA WA TAIFA KIMATAIFA KAMA SISI

admin August 8, 2019 2:19 pm


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hakuna rekodi ambayo imewahi kuvunjwa na timu yoyote ya kujaza uwanja wa Taifa mapema tangu walipofanya wao Julai 28 mwaka 2016 kwenye michuano ya kimataifa ambapo Yanga ilicheza na TP Mazembe.

Yanga imesema kuwa kwenye mchezo huo mapema saa 6 mchana walikuwa wamejaza uwanja huo na mageti yote kufungwa ili kuzuia mashabiki waliokuwa nje wasiingie ndani.

Barabara zote zilijaa wananchi na ilibidi zifungwe na Polisi walitumika kuzuia wananchi wasiingie ndani ya uwanja na kuwatuliza wale waliokuwa nje.

Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa kwa sasa mashabiki wanatakiwa wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa siku ya jumamosi kushuhudia ushindani kati yao na wapinzani wao Township Rollers uwanja wa Taifa.

TOTTENHAM WANAHAHA KUMPATA DYBALA SIMBA HAWALALI, WAICHANA YANGA KIMTIDO, YADAI IMEWAPOTEZA MAZIMA KWENYE MAPATO NA MASHABIKI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply