Uncategorized

KMC SIO WA MCHEZOMCHEZO, WAMFUATA HARUNA NIYONZIMA WA SIMBA KIBABE

admin August 9, 2019 12:34 am


KIKOSI cha KMC, hakitaki kabisa utani kimataifa kwani jana kimewafuata wapinzani wao kibabe wakiwa wametupia mavazi matata.

KMC inapeperusha Bendera ya Tanzania Kimataifa ambapo Agosti 10 itatupa karata yake ya kwanza mbele ya AS Kigali ya Rwanda.

Kwenye timu ya AS Kigali yupo nyota wa zamani wa Simba, Haruna Niyonzima ambaye amesajiliwa msimu huu baada ya kandarasi yake kuisha ndani ya Simba.

Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa umakini wao kwa kila jambo unawafanya wajiamini kwamba watafanya vizuri.

“Kila kitu kipo kwenye mpangilio sahihi, hata aina ya mavazi pia tumejipanga kwa kuwa tunawakilisha nchi kimataifa, mashabiki watupe sapoti tutafanya vema,” amesema Binde.

Tayari kikosi kipo Rwanda na jana kimeanza kufanya mazoezi ya awali kabla ya kuwavaa wapinzani wao kimataifa.

YANGA YATOSHANA NGUVU NA MALINDI, WACHOMOA BAO DAKIKA ZA USIKU UONGOZI WA YANGA WAKOMELEA MSUMARI ISHU YA JUMA ABDUL, DANTE NA YONDAN

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply