Uncategorized

AZAM FC KUTUPA KARATA YAO YA KWANZA LEO KIMATAIFA

admin August 11, 2019 10:29 am


AZAM FC, leo wana kazi ya kutupa kete ya kwanza mbele ya Fasil Kenema nchini Ethiopia kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa majira ya saa 10:00.

Kwa timu za Tanzania ambazo zinashiriki michuano ya kimataifa zote jana zilikamilisha kuchanga karata ya kwanza kabla ya mechi za marudio ambapo hakuna hata timu moja iliyopata ushindi zaidi ya kuambulia sare.

Yanga ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 nyumbani Uwanja wa Taifa mbele ya Township Rollers na Simba nao mbele ya UD Songo ugenini walilazimisha sare ya bila kufungana.

KMC ililazimisha sare ya bila kufungana ugenini mbele ya AS Kigali ya Rwanda.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo.

TANZANITE YABEBA KOMBE LA COSAFA, YALIPA KISASI KWA ZAMBIA LEO ARSENAL KUANZISHA MASHINE ZAKE MPYA LEO MBELE YA NEWCASTLE UNITED

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply