Uncategorized

TANZANITE YABEBA KOMBE LA COSAFA, YALIPA KISASI KWA ZAMBIA LEO

admin August 11, 2019 10:09 am

TIMU ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ leo imetwaa ubingwa wa michuano ya COSAFA nchini Afrika Kusini baada ya kulipa kisasi mbele ya Zambia.

Tanzanite iliyo chini ya Kocha Mkuu Bakari Shime kwenye hatua ya makundi ilipokutana na Zambia ilifungwa mabao 2-1 na leo wamerejesha mabao na kusepa na kombe lao licha ya kualikwa kwenye michuano hiyo.

Mabao kwa upande wa Tanzanite yalipachikwa na Opa Clement dakika ya 24 pamoja na Protasia Mbunda aliyefunga dakika ya 87 Uwanja wa Wolfson Port Elizabeth.

SIMBA WAIKOMALIA YANGA, WAIPA TANO KISHA KUICHANA KIMTINDO AZAM FC KUTUPA KARATA YAO YA KWANZA LEO KIMATAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply