Uncategorized

SIMBA WAIKOMALIA YANGA, WAIPA TANO KISHA KUICHANA KIMTINDO

admin August 11, 2019 6:34 am


UONGOZI wa Simba umesema kuwa Yanga wanastaihili pongezi ila wamewaangusha wananchi kwa kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Township Rollers jana uwanja wa Taifa.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa, kazi kubwa ambayo Yanga walipaswa waifanye ni kupata matokeo chanya kwa kuwa walikuwa nyumbani.

“Hongereni Yanga kwa kupata sare ya nyumbani ila haijawa sawa kwa Wananchi kwa kuwa mlikuwa na sapoti ya mashabiki na imekuwa ngumu kuitumia.

“Raha ya mchezo wa nyumbani ni kuwa na mashabiki, hivyo tutawaonyesha namna ya kufanya kwenye mchezo wetu wa marudio,” amesema. 

Simba jana ililazimisha sare tasa dhidi ya UD Songo ya Msumbiji mchezo wao marudio unatarajiwa kuwa kati ya Agosti 23-25 uwanja wa Taifa na Yanga nao watakuwa ugenini nchini Botswana.

ZAHERA AFICHUA KINACHOIMALIZA YANGA, APANIA KUPETA UGENINI TANZANITE YABEBA KOMBE LA COSAFA, YALIPA KISASI KWA ZAMBIA LEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply