Uncategorized

ZAHERA AFICHUA KINACHOIMALIZA YANGA, APANIA KUPETA UGENINI

admin August 11, 2019 4:34 am


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa bado kikosi chake hakijawa na maelewano mazuri jambo ambalo liliwapa taabu kupata matokeo kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Township Rollers.

Yanga jana imelazimisha sare dhidi ya Township Rollers, mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa kwa kufungana bao 1-1.

Mchezo wa marudiano wa kimataifa unatarajiwa kuchezwa  kati ya Agosti 23-25 nchini Botswana.

“Wachezaji wangu bado wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kuelewana wakiwa ndani ya uwanja jambo ambalo linaleta ugumu kwenye kupata matokeo uwanjani.

“Kwa sasa hesabu ni kuona kwamba tunakuwa na kikosi imara ambacho kitapata matokeo kwenye mchezo wetu wa marudio, mashabiki waendelee kutupa sapoti katika hili, nami nitafanyia kazi makosa yote,” amesema.

SIMBA WAREJEA BONGO KUIWAHI AZAM FC SIMBA WAIKOMALIA YANGA, WAIPA TANO KISHA KUICHANA KIMTINDO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply