Uncategorized

PAUL POGBA BADO PASUA KICHWA NDANI YA UNITED

admin August 13, 2019 7:04 am


PAUL Pogba, kiungo wa Manchester United amefungua mjadala mpya juu ya ishu yake ya kutaka kutimka ndani ya kikosi hicho.

Pogba kabla ya msimu alisema wazi kuwa anahitaji kupata changamoto mpya jambo ambalo liliwafanya mabosi wa United kutumia nguvu kubwa kumbakisha ndani ya kikosi hicho.

Nyota huyo alikuwa ndani ya kikosi kilichowapa maumivu Chelsea, Old Trafford kwa ushindi wa mabao 4-0 na alitoa pasi moja ya bao matata sana umbali wa yadi 70 bao likipachikwa na Marcus Rashford.

Pogba bado amesisitiza anataka kusepa ndani ya kikosi hicho.”Hata kama tumeanza msimu ni muda wangu wa kupata changamoto mpya.


 “Kiukweli kuna mambo ambayo nimeyasema ila kwa sasa ni jambo la kusubiri muda utazungumza. Hili litabaki kuwa swali hata kama nimesema nipo ndani ya Manchester United na ninafurahi kucheza na wanzangu na kuona tunapata matokeo,” amesema.

Real Madrid inapewa chapuo ya kumbeba nyota huyo licha ya dirisha kufungwa.

SERIKALI YAIPA TANO ZA KUTOSHA TANZANITE YANGA YAENDA CHIMBO KUTAFUTA DAWA YA TOWNSHIP ROLLERS

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply