Uncategorized

SIMBA:TUNAITAKA NGAO YA JAMII, TUTAPAMBANA MBELE YA AZAM FC

admin August 15, 2019 7:09 am


UONGOZI wa Simba umesema kuwa hakuna namna yoyote ile watakayofanya mbele ya Azam FC kwenye mchezo wao wa ngao ya jamii zaidi ya kushinda na kutwaa ngao hiyo.

Simba itashuka uwanja wa Taifa, Agosti 17 kumenyana na Azam FC kwenye mchezo huo maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 23.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa hakuna kingine ambacho wanakiwaza kwa sasa zaidi ya kutwaa ngao ya jamii.

“Tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu kwetu nasi tunajipanga kufanya vema mbele ya wapinzani wetu Azam Fc, ni timu bora na makini ila hakuna namna tunahitaji ushindi na kutwaa ngao ya jamii,” amesema.

AZAM FC YAANZA KUIWINDA SIMBA, YAPANIA KUFANYA MAAJABU YANGA YAKUBWA NA MSALA, MAKOMANDOO WAJIONDOA, WAANDIKA BARUA, IDADI KAMILI HII HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply