AUSTRIA YAIGOMEA ALGERIA ZIKIFUZU HATUA YA MTOANO
Algeria na Austria zimefanikiwa kufuzu hatua ya mtoano baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi uliokuwa na ushindani mkali.
Algeria ilikaribia kusawazisha bao hilo dakika ya 36 lakini shuti la Ibrahim Maza likagonga mwamba na kurudi uwanjani.
Dakika ya 45, Algeria ikafanikiwa kusawazisha bao hilo likifungwa na beki, Rafik Belghali, aliyewatoka mabeki wa Austria na kuachia shuti kali, timu hizo zikaenda mapumziko kwa sare ya bao 1-1.
Kipindi cha pili, kiungo Marcel Sabitzer alifanikiwa kuirudisha Austria kwenye uongozi akifunga bao kwa shuti kali, akipokea pasi safi kutoka kulia ya Konrad Laimer.
Algeria ikafanikiwa kusawazisha tena dakika ya 60 kwa bao la shuti kali kutoka kwa winga na nahodha wake, Riyad Mahrez akipokea pasi nzuri ya Houssem Aouar kutoka upande wa kushoto.
Mahrez tena akafunga bao la tatu ambalo kwake lilikuwa la pili dakika ya 90+3 akitengenezewa na yuleyule Aouar akiitanguliza Algeria kwa mara ya kwanza kwenye mchezo huo.
Matokeo hayo yanalifanya kundi J kuongozwa na Argentina iliyomaliza na pointi tisa, ikifuatiwa na Austria na Algeria kila moja ikiwa na pointi nne, wakati Jordan haina kitu.
Algeria sasa itakwenda kukutana na Uswizi kwenye mchezo wa mtoano huku Austria ikikutana na Hispania, wakati Argentina ikiikabili Cape Verde.