Uncategorized

AZAM FC YAANZA KUIWINDA SIMBA, YAPANIA KUFANYA MAAJABU

admin August 15, 2019 6:29 am


AZAM FC tayari wameanza maandalizi ya kuiwinda Simba kwenye mchezo wa ngao ya jamii utakaochezwa Agosti 17 uwanja wa Taifa.

Mchezo huo maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 23 utachezwa majira ya saa 1:00 usiku.

Jaffary Maganga, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ushindani mbele ya Simba.


Mchezo wa ngao ya jamii huwakutanisha mabingwa wa msimu, ambapo Simba ni kwa upande wa Ligi Kuu Bara huku Azam FC wakiwa ni mabingwa wa kombe la Shirikisho.

Msimu uliopita Simba ilitwaa ngao hiyo mbele ya Mtibwa Sugar kwa ushindi wa mabao 2-1.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTIXTRA ALHAMISI SIMBA:TUNAITAKA NGAO YA JAMII, TUTAPAMBANA MBELE YA AZAM FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply