Uncategorized

NJEMBA ANASWA NA VIDEO 555 ZA NGONO

admin August 22, 2019 4:14 pm


RAIA mmoja wa Colombia ambaye jina lake halikutajwa, ameshikwa na polisi wa Hispania akiwa na video 555 zenye kuonyesha sehemu za siri za wanawake ikiwa ni pamoja na nguo zao za ndani.

Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 53 alichukua video hizo jijini Madrid, Hispania, kwa siri akitumia kidude maalum (cellphone) alichokuwa anakiweka chini ya miguu ya wanawake waliokaa au waliosimama, kikachukua taswira ya ndani ya wanawake hao katikati ya miguu yao.

Wanawake waliolengwa ni wale waliokuwa wanasafiri kwenye treni  wakiwa wamekaa au kusimama, na kwenye maduka makubwa (supermarket).

Polisi nchini Hispania wanasema video hizo zilizokuwa zikionyesha taswira za wanawake wakiwemo watoto wadogo zilianza kusambaa mnamo Julai 2018 kwenye tovuti.

Katika njama hizo mtu huyo alipata wafuasi 3,519, watembeleaji 84,594 na kufanya idadi nzima ya watu walioangalia video hizo kufikia 1,367,999.

FAMILIA YAPINGA MAHAKAMANI WOSIA WA MENGI, MAZITO YAIBUKA KIUNGO WA RWANDA AIPA USHINDI SIMBA YA MBELGIJ MBELE YA UD SONGO, ATAJA SABABU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply