Uncategorized

YANGA: BADO TUPO SANA KIMATAIFA, ZESCO WETU KABISA

admin August 26, 2019 5:32 am


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa unajipanga kwa ajili ya mchezo wao wa hatua ya mtoano dhidi ya Zesco utakaopigwa mwezi ujao kati ya Septemba 13-15.

Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa wana imani kubwa ya kufanya vema kutokana na ubora wa kikosi walichonacho.

Akizungumza na Saleh Jembe, Msolla amesema kuwa kwa sasa mpira una mabadiliko makubwa na mipango mikubwa inawezekana.

“Tupo vizuri na tuna imani ya kufanya vema kimataifa, kwa sasa hatuna presha kwani hata tukitolewa kwenye hatua hii tuliyopo tutadondokea kombe la Shirikisho, tutaendelea kuwa kimataifa,” amesema.

Yanga imerejea usiku wa kuamkia leo ikitokea nchini Botswana ikiwa na ushindi wa bao 1-0 na imesonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1.

MOHAMED SALAH NI WA MOTO EPL, ARSENAL HAWANA BAHATI NAYE KABISA BALINYA APOKELEWA KIFALME YANGA, AWEKEWA ULINZI MKALI – VIDEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply