Uncategorized

RONALDO AWAPAISHA JUVENTUS INSTAGRAM

admin August 29, 2019 9:07 pm

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na Klabu ya Juventus ya Italia, Cristiano Ronaldo, amekuwa kivutio kwa timu yake huku akiiongezea wafuasi milioni 20 Instagram baada ya kuikacha timu yake ya zamani, Real Madrid.


Kabla ya ujio wa mshambuliaji huyo timu hiyo ilikuwa na wafuasi milioni 10 Instagram na kwa sasa imefikisha wafuasi milioni 31 na kuwa kati ya klabu tano duniani zenye wafuasi wengi Instagram.

Timu zenye wafuasi wengi Instagram ni:

1. Real Madrid –  wafuasi milioni 77.6

2. Barcelona – mil. 76.4

3. Juventus – mil. 31.1

4. Manchester United – mil. 31

5. PSG – mil. 23.8

Wafuasi wa Instagram wamekuwa wakidai kupitia mtandao wa kijamii kuwa mvuto wa timu hiyo umeongezeka zaidi baada ya kuwasajili wachezaji wanane wenye viwango vya juu ambao ni Matthijs de Ligt, Danilo, Cristian Romero, Luca Pellegrini, Merih Demiral, Adrien Rabiot, Aaron Ramsey na Gianluigi.

PROF JAY NA P FUNKY KIMENUKA KISA MPUNGA WALIOOA FC WACHEKELEA SAPOTI YA SALEH JEMBE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply