Uncategorized

DUH! DIJK ALIWAKIMBIZA MARA TATU KWA KURA CR 7 NA MESSI

admin September 1, 2019 12:35 am


IMEELEZWA kuwa nyota wa Liverpool, Virgil Van Dijk ambaye amebeba tuzo kubwa ya kuwa Mchezaji Bora wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) aliwaacha kwa mbali wapinzani wake wa karibu aliokuwa akipambana nao.

Kwenye usiku wa tuzo za UEFA, Dijk alisepa na tuzo mbili ambapo alianza kutwaa ya beki bora kaba ya kusepa na ile iliyokuwa ikitazamwa na wengi ya Mchezaji Bora wa Ulaya.

Kipa wake Allison alisepa na Tuzo ya Kipa Bora wa UEFA huku wakongwe katika gemu, Lionel Messi na Cristiano Ronado wakiachwa mbali kwa kura.

Dijk alikuwa msaada mkubwa kwa kuiwezesha Liverpool kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita inaelezwa kuwa alipata kura mara tatu zaidi ya washindani wake.

Kwa tuzo hiyo anakuwa ni Mholanzi wa kwanza kushinda tuzo hiyo kubwa kwa wachezaji wa kiume.

HIVI NDIVYO MWENDO WA MANCHESTER UNITED KWA SASA EPL KUMBE SIMBA ILITOLEWA KIMAKOSA CAF

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply