Uncategorized

DUH! KUMBE LUGHA TATIZO KUBWA KWA VIFUAVIWILI

admin September 9, 2019 10:03 pm

BRUNO Tarimo ‘Vifuaviwili’ bondia wa ngumi za kulipwa ambaye ni  bingwa wa International Super Feather Weight ambao ameupaata hivi karibuni nchini Serbia kwa kumtwanga kwa pointi bondia Scheka Gurdijeljac raia wa Serbia amesema kuwa ishu inayompasua kichwa ni lugha tu.

Vifuaviwili amesema kuwa kila anaposkia kuna pambanao mbele yake nje ya nchi hata ndani hana mashaka ya kupata ushindi kinachompa ugumu ni mawasiliano hasa wa lugha za kigeni kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha.

“Unajua elimu yangu mimi darasa la saba sasa ninapokuwa na kazi nje wao hawajui Kiswahili kabisa wala kiingereza ambacho ninakijua mimi kuna wengine hawajui hapo ndio tatizo lilipojificha na huwa ninapata taabu kidogo.

“Ila kikubwa ambacho kinanifanya nielewe huwa ninakuwa na mtu ambaye ni mtaalamu wa lugha yeye ananisaidia kuelewa na nikikaa sehemu kwa muda kidogo huwa naweza kujibadili kutokana na mazingira ili kuelewa kinachozungumzwa,” amesema Vifuaviwili.

KASEJA TUNAMSIFIA LAKINI TUKUMBUKE TULIPOMTENGA ILI TUSIRUDIE KWA WENGINE KAPTULA YA ZAHERA HAIWEZI KUWA ISHU, TWENDENI NA MAMBO YA MSINGI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply