Uncategorized

NAHODHA SIMBA: TUNAWATAMBUA AZAM FC TUTAWAPA TAABU LEO

admin January 10, 2020 1:01 pm


NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa hana mashaka na mchezo wa leo mbele ya Azam FC utakaochezwa Uwanja wa Amaan.

Simba itamenyana na Azam FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi atakayefungwa leo anafungashiwa virago na kurejea Bongo na mshindi atamenyana na Mtibwa Sugar ambaye ameshakata tiketi yake jana, Januari 9, mbele ya Yanga.

“Ninatambua utakuwa mchezo mgumu ila hakuna cha kuhofia mbele ya Azam FC, tutapambana kufikia malengo yetu na tupo tayari kwa ajili ya kupata ushindi, mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Azam FC ina kumbukumbu ya kuitungua Simba mwaka 2019 mabao 2-1 kwenye mchezo wa hatua ya fainali, wanakutana leo wakiwa ni mabingwa watetezi na mshindi wa pili.

NAHODHA WA BARCELONA AWA MKALI KINOMA, AKASIRISHWA NA ZAWADI YA KICHAPO MBELE YA ATLETICO MADRID ISHU YA YANGA KUIKIMBIA SIMBA KIJANJA MAPINDUZI CUP IPO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply