Uncategorized

ISHU YA YANGA KUIKIMBIA SIMBA KIJANJA MAPINDUZI CUP IPO HIVI

admin January 10, 2020 1:01 pm


KUTOKANA na mashabiki wa Yanga kukasirika kitendo cha Yanga kupoteza mchezo wao wa nusu fainali kwenye Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa Sugar huku ikielezwa kuwa ni ujanja wa kuikimbia Simba uongozi wa Yanga umesema kuwa hakuna kitu kama hicho.

Yanga ilianza kufunga bao la kuongoza kwenye mchezo huo kupitika kwa Deus Kaseke jana Uwanja wa Amaan lilisawazishwa na Mtibwa Sugar dakika ya 90+2 na Shomari Kibwana na kupelekea kufungwa kwa penalti 4-2.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa hawaiogopi timu yoyote ni upepo tu haukuwa kwao jana.

“Tunacheza kwa malengo, wachezaji wamepambana kwa hali na mali mwisho wa siku tumefungwa usiku kutokana na makosa ya wachezaji wetu na bahati kuwa kwa Mtibwa Sugar.

“Upande wa penalti hazina mwenyewe tunarudi Bongo kujiaandaa na ligi, kuna mengi ya kufanya mashabiki watupe sapoti na hatujawakimbia Simba sisi,” amesema.

Yanga wamerejea leo Bongo wakitokea Visiwani Zanzibar na wamewaacha wababe wao Mtibwa Sugar wakisubiri mshindi wa pili kati ya Azam ama Simba ili wacheze nao fainali, Januari 13.

NAHODHA SIMBA: TUNAWATAMBUA AZAM FC TUTAWAPA TAABU LEO JEMBE JIPYA LA AZAM FC KUIKOSA SIMBA LEO MAPINDUZI CUP

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply