Uncategorized

MTAMBO MPYA YANGA SASA UPO FITI

admin January 12, 2020 9:36 pm

STRAIKA mpya wa Yanga, Tariq Seif, yupo fiti baada ya kupona majeraha ya nyama za paja yaliyomfanya akae nje kwa siku kadhaa.

Tariq aliyejiunga na Yanga katika usajili wa dirisha dogo, alipata majeraha hayo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara msimu huu dhidi ya Biashara United ambapo alifunga bao katika ushindi wa 1-0.

Daktari wa Yanga, Sheck Mngazija, alisema: “Tariq tayari ameshakuwa sawa baada ya kufanyiwa matibabu.

“Baada ya kupona kwake, hivi sasa hakuna majeruhi yeyote kwa timu yetu, hivyo wachezaji wote wa Yanga wapo fi ti kwa ajili ya kucheza.”
TAZAMA MABAO YA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE ‘TANZANIA VS BURUNDI’ (5-1) VIDEO KAKOLANYA ATOA TAMKO JUU YA NAFASI YAKE SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply