Uncategorized

MRITHI WA MAYANJA NDANI YA KMC HUYU HAPA, AANZA KAZI

admin January 14, 2020 9:27 am

 HARUNA Harerimana ameingia mkataba na KMC kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo kwa kandarasi ya mwaka mmoja na miezi nane.

 Harerimana anachukua nafasi ya kocha Jackson Mayanja  aliyestishiwa mkataba wake kutokana na timu kutokuwa na matokeo mazuri kwenye ligi na Kimataifa.

Harerimana amepitishwa na Bodi ya timu ambayo ilipitia maombi mengi ya makocha wa ndani na nje ya nchi.

Harerimana alikuwa akiinoa Lipuli, ametambulishwa kwa wachezaji na tayari ameanza kazi ya kuinoa timu ya KMC kwa ajili ya mashindano ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam.
Benjamin Sitta, Mwenyekiti wa Bodi ya KMC amesema kuwa wana imani na kocha huyo atarudisha morali na hali ya kujiamini kwa timu.

Mechi ya kwanza ya Harerimana itakuwa dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Uhuru na katika mchezo wa kombe la Azam.

POLISI TANZANIA YAMDAKA KIPA WA SIMBA, YAMPA MWAKA MMOJA SITA WAPIGWA CHINI JUMLA NDANI YA KMC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply