Uncategorized

BOSI WA LIVERPOOL ALITUMIA DAKIKA 15 KUWARUDISHIA FURAHA NYOTA WAKE MANE NA SALAH

admin January 17, 2020 5:32 am
JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa alimaliza mapema mgogoro wa nafsi kati ya Mohamed Salah na Sadio Mane uliotokea ndani ya timu yake mwezi Agosti,2019.
Mshambuliaji Sadio Mane alionekana kumlalamikia Salah kwa kushindwa kumpa pasi ya wazi wakati akitoka alipofanyiwa mabadiliko.
Kwenye mchezo huo dhidi ya Burney uliochezwa Uwanja wa Turf Moor, Salah aliamaua kupiga shuti badala ya kutoa pasi na timu yake ilishinda mabao 3-0.
Klopp amesema kuwa:” Kwenye mpira kuna maajabu sana unaweza kumtazama mchezaji namna anavyofanya na ukapata maneno rasmi anayoongea, niliona kama Mane amesema ‘Ohh kwa nini umeamua kufanya hicho ulichofanya,? ila ni maisha ya mpira na yote lazima yatokee.
“Haikunichukua muda mrefu  baada ya mechi nilikaa nao wote na nikazungumza nao kwa muda usiopungua dakika 15, na sasa unaona wana furaha na masiha yanaendelea,” amesema.
RASHFORD HATIHATI KUIKOSA LIVERPOOL, NDANI YA CHAMPIONI IJUMAA BEKI WA MANCHESTER UNITED ASHINIKIZA KUSEPA MAZIMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply